ARUSHA
Mwili
wa mtoto ambaye anakadiriwa kuwa na umri wa siku moja umeokotwa kwenye mfereji
wa kupitisha maji machafu katika eneo la Mtaa wa Ali Nyanya kata ya Ungalimited
jijini Arusha.
Kichanga
hicho kimeonekana kutekelezwa na mama yake mzazi mara tu baada ya kujifungua na
kupelekea kupoteza maisha
Baadhi
ya wananchi wa eneo hilo wamelaani kitendo hicho cha kinyama na kikatili
kinachofanywa na baadhi ya wanawake wasiokuwa na hofu ya Mungu ndani yao ambao
wanakatisha uhai wa watoto hao ambao hawana hatia.
Mwenyekiti
wa Mtaa huo Omari Shehe naye amelaani kitendo hicho na kuahidi kushirikiana na
vyombo vya dola kuhakikisha wanamtafuta muhisika ambaye amefanya tukio hilo la
kinyama ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia hizo za kufanya uovu na
ukatili huo.
Vitendo
vya watu kutekeleza watoto vimekuwa vikishamiri katika maeneo mbalimbali ya
nchi huku wengi wakionekana kufanya ukatili huo kutokana na baadhi ya wanaume
kukataa watoto au ujazito jambo ambalo hata hivyo halikubaliki.
No comments:
Post a Comment