Picha kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda B.Lilian Charles Matinga |
MPANDA.
Mkuu wa wilaya ya
Mpanda Bi. Lilian Charles Matinga amewataka wananchi wa wilaya ya Mpanda Mkoani
Katavi kutii sheria bila shurti kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za
nchi.
Bi Matinga amesema hayo
leo ofisini kwake wakati akizungumza na Mpanda redio na kubainisha kuwa ofisi
yake imetenga siku ya Jumanne na Alhamisi kila juma kwa ajili ya kusikiliwa
matatizo ya wananchi.
Katika kuendelea
kuhimiza utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika jamii Bi Matinga amesema
amefanya mikutano katika kata zote wilayani Mpanda ambapo pia amesikiliza
matatizo ya wananchi.
CHANZO: MDAKI HUSSEIN.
No comments:
Post a Comment