KAGERA.
Wanafunzi 9 wa shule ya msingi Kihinga mkoani Kagera
wamefariki dunia na wengine zaidi ya 25 kujeruhiwa baada ya kulipukiwa na bomu.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera Agustino
Olomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema kwamba wanafunzi hao
walikuwa wakati wa mapumziko ya saa nne, na ndipo mlipuko huo ulipotokea na
kusababisha madhara makubwa ya vifo.
Kamanda Olomi amesema tayari wananchi
wamejitokeza kuchangia damu kwa ajili ya kuwasaidia majeruhi.
Kwa mujibu wa Dokta Mariagoreth Fredrick ambaye ni
mganga mkuu hosipitali ya Rurenge, amethibitisha kupokea miili hiyo na majeruhi
ambao baadhi wako katika hali mbaya na tayari wanapatiwa matibabu.
Inaelezwa kwamba kabla ya kulipukiwa na kifaa hicho
kinachoarifiwa kuwa ni bomu, wanafunzi hao walikuwa wanakichezea bila kujua ni
hatari.
CHANZO: EA TV.
No comments:
Post a Comment