Thursday, 14 December 2017

Miili ya Askari wa JWTZ waliouawa DRC imeaagwa kwa ajili ya mazishi.



DAR ES SALAAM

Miili ya asikali 14 walio uawa katika shambulio la kundi la waasi nchini Kongo imeaagwa kwa ajili ya mazishi.
Waziri Mkuu wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kasimu  Majaliwa  amesema serikali imeutaka umoja wa mataifa kufanya uchunguzi wa kina kuhsu shambulio lililopoteza askali kumi 14 wa Tanzania.
Sanajari na hayo Mkuu wa Majeshi CDF Venance Mabeyo amesema majeruhi 44 wanaendelea na matibabu katika miji ya Kampala Kinshansa na Goma huku askali mmoja akiwa bado hajapatikana.
Mara baada ya shughuri za kuuaga miili ya asikali hao katika viwanja vya Jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ imesafirishwa kuelekea mikoani waliko zaliwa kwaajili ya mazishi. 
Wanajeshi 14 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ), waliouawa katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wakati wakilinda amani Haya ni majina yao.
Wanajeshi hayo ni  Hamad Haji Bakari, Chazil Khatibu Nandonde, Idd Abdallah Ally, Juma Mossi Ally,  Ally  Haji Ussi, Pascal Singo, Samwel Chenga, Deogratius Kamili, Mwichumu Vuai Mohamed, Hassan Makame, Issa Mussa Juma, Hamad Mzee Kamna, Salehe Mahembano na Nazoro Haji Bakari.
Tayari miili ya marehemu hao imeshaagwa katika viwanja vya ulinzi vilivyopo makao ya jeshi yaliyopo Upanga jijini Dar es Salaam na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na viongozi wa Serikali wengine waliongoza Watanzania kutoa heshima za mwisho kwa askari hao.
Askari hao 14 walifariki dunia katika mapigano na waasi wa kikundi cha ADF nchini DRC, huku 44 wakijeruhiwa na mmoja akipotea baada ya kambi yao kuvamiwa eneo la Mashariki mwa nchi Desemba 7 wakati wakitekeleza majukumu ya ulinzi wa amani.
Chanzo:mwananchi


No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...