Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu |
DAR ES SALAAM
Takwimu hizo za Januari hadi Novemba zinaonyesha
mkoa wa Mbeya umekuwa na wagonjwa 710 na vifo 14 huku Songwe ikiwa nao wagonjwa
538 na vifo vinne.
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameitaja mikoa
mingine iliyoathirika zaidi kuwa ni Morogoro , Dar es Salaam .Iringa na Kigoma
.
Aidha amefafanua kuwa takwimu za tangu mwaka huu
uanze zinaonyesha ongezeko la ugonjwa ambapo mikoa 17 ilitoa taarifa za kuwapo
kwa wagonjwa.
Hata hivyo, amesema mikoa saba haikuripoti kuwa
na ugonjwa huo ikiwamo Mwanza, Shinyanga, Arusha, Lindi, Kagera, Simiyu,
Kilimanjaro na Mtwara.
SOURCE:
EATV.
No comments:
Post a Comment