Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga ameweka jiwe la msingi katika kiwanda cha maziwa cha Kashaulili Livestock Keepers Saccos kinachojengwa katika kata ya Makakanyagio Halmashauli ya Manispaa Mpanda.
Katika uzinduzizi huo,Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa Katavi kujitokeza kwa wingi kuwekeza viwanda ili kujenga Tanzania ya viwanda kama serikali ya awamu ya tano ilivyoagiza.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kiwanda hicho chenye wanachama zaidi ya 50 Andrea Fumbi amesema,kiwanda hicho kitagharimu zaidi ya shilingi milioni 600 kwa udhamini wa Benki ya TIB,ambapo kinatarajia kuzalisha maziwa ifikapo September mwaka huu.
Wakati huo huo Afisa mazingira Manispaa ya Mpanda Bw.Said Mandua pamoja na mambo mengine amewatoa hofu usalama wa mazingira katika makazi wakazi wa Manispaa ya Mpanda kutokana ujenzi wa kiwanda hicho ambacho kipo nje kidogo ya mita 60 kutoka chanzo cha mto mpanda.
Mpaka sasa Mkoa wa Katavi una viwanda viwili vya maziwa ambapo kimoja kilichopo kata ya Ilembo kilizinduliwa na na mwenge wa uhuru mwezi April mwaka huu.
No comments:
Post a Comment