Wednesday, 7 March 2018

UNUNUZI WA GARI LA TAKA LA MANISPAA YA MPANDA HAUPASWI KUWA KAMA ZAWADI KWA WANANCHI.


Gari la taka lahalmashauri ya wilaya ya Mpanda lililonunuliwa.

MPANDA.

Mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Rhoda Kunchela  mkoa wa Katavi amesema ununuzi wa gari la taka la Manispaa ya Mpanda haupaswi kuwa kama zawadi  kwa wananchi.

Katika mahojiano na Mpanda Redio mbunge huyo amesema kubadili matumizi ya fedha zilizokuwa kwa ajili ya manunuzi ya gari la meya wa manispaa na kununua gari ya taka hakufuti dhana ya fedha kuwa za mlipa kodi.

Katika hatua nyingine amemtaka mstahiki meya wa manispaa ya Mpanda Willium Mbogo kutoa ufafanuzi wa fedha zaidi ya million 90 zilizotolewa awali kwa ajili ya manunuzi ya gari la taka .

Mwezi mmoja uliopita Halmashauri ya manispaa ya Mpanda  ilinunua gari la taka kwa gharama ya shilingi milioni 159 ili kupunguza kero ya taka katika manispaa.

Chanzo:Rebecca Kija

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...