Picha ya jengo la shule lililoezuliwa na upepo. |
MPANDA.
Zaidi
ya wanafunzi 268 wa shule ya msingi mwamkulu kata ya mwamkulu manispaa ya
mpanda wanalazimika kusomea chini ya miti baada ya mvua kubwa iliyoambatana
na upepo kuezua paa la shule hiyo.
Diwani
wa kata ya mwamkulu Kalipi Katani ameiambia Mpanda Radio kuwa mvua hiyo
imenyesha siku ya tarehe 4 mwezi 3 mwaka huu imeezua paa la darasa moja na
jengo la ofisi mkuu wa shule hiyo.
Licha
ya shule mvua hiyo pia imeharibu majengo kadhaa ikiwemo maghala ya mazao
mawili, kanisa lililokuwa likitumiwa na wanafunzi wa darasa la awali na nyumba
ya mwenyekiti wa mtaa wa nguvumali.
Kutokana
na hali hiyo kamati ya shule imeitisha mkutano wa wazazi wa shule hiyo na
pamoja wameridhia kuchangia ukarabati wa darasa na jengo ofisi ya mkuu wa shule
hiyo ambapo diwani wa kata hiyo amechangia sh. laki moja (100,000/=) kwa ujenzi wa shule na
kumchangia sh. elfu hamsini (50,000) mwenyekiti aliyekumbwa na maafa hayo.
Source:Haruna Juma
No comments:
Post a Comment