Tuesday, 6 March 2018

MKUU WA WILAYA YA MPANDA AMEWATAKA WASIMAMIZI WA ZOEZI LA UANDIKISHWAJI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA KUFANYA KAZI KIZALENDO.

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi Mh. Lilian Matinga


MPANDA.

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi Lilian Matinga amewataka wasimamizi wa zoezi la uandikishwaji wa vitambulisho vya taifa kufanya kazi kizalendo kwa kufuata kanuni na sheria za Jamuhuri ya Tanzania.

Wito huo ameutoa leo  wakati  wa zoezi la uapishwaji wa wasimamizi hao ameeleza  kusema kuwa kufanya hivyo kutawafanya wafanye kazi zao kwa weledi mkubwa bila kupendelea upande mmoja.

Kwa upande wao baadhi ya wasimamizi hao wamesema kuwa watafanya kazi kwa umakini na kwa kujitoa ili kuweza kukamilisha zoezi hilo kwa usalama na kwa wakati uliopangwa.

Zoezi la uandikishwaji vitambulisho linatarajia kuanza hivi karibuni ambalo litawapa wananchi fursa ya kujipatia vitambulisho vya kudumu vya uraia wa Tanzania.

Chanzo:Furaha Kimondo


No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...