KATAVI
Jaji mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Khamisi Juma
Mahakama ya hakimu mkazi
Mkoa wa Katavi imepokea waraka kutoka kwa jaji mkuu wa Tanzania Profesa
Ibrahim Khamisi Juma unaokataza Tozo ya malipo kwa hati za hukumu ambazo ilikuwa inatozwa kwa wananchi .
Hayo yamebainishwa na Afisa mawasiliano na Tehama wa
mahakama hiyo Jemes Vedasi Kapele wakati akizungmza na mpanda redio amesema waraka huo unaelekeza usitishwaji wa
tozo za hati za hukumu.
Aidha kapele amesema kufutwa kwa tozo hizo kutasaidia
wanachi wenye uchumi mdogo ambao walikuwa wanashidwa kulipia hati za hukumu
kutokana na ukosefu wa fedha hali iliyokua inapelekea kushindwa
Kupata haki zao.
Hivi karibuni akiwa ziarani mkoani Kigoma jaji mkuu
prof.Ibrahim Khamis Juma alitoa tamko la kusitisha malipo ya hati za hukumu.
Source:paul mathias
No comments:
Post a Comment