Monday, 19 March 2018

WANANCHI WILAYANI MPANDA WALIA NA KERO YA MAJI


MPANDA


Wananchi wa manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wameiomba serikali kutatua kero ya maji wanayokumbana nayo ili kupunguza adha hiyo.
Wameyasema hayo wakati wakizungumza na Mpanda radio na kusema kuwa katika kuadhimisha wiki ya maji nchini  tatizo la maji limekuwa ni tatizo sugu  na kuwalazimu kutembea umbali mrefu ili kuweza kupata  maji katika visima na mito hali inayohatarisha usalama wao.
Maeneo mengi katika manispaa ya Mpanda yamekumbwa na kero ya maji ambapo kwa kila wiki maji hupatikana kwa siku tatu na hutoka kwa masaa matatu mpaka manne na kupelekea wananchi wengi kukosa maji.
Wiki ya maji kitaifa huadhimishwa kila tarehe22 march ambapo kwa mwaka huu imebebwa na kauli mbiu inayosema hifadhi maji na mfumo wa kiiokolojia kwa maendeleo ya jamii.
Chanzo:Ezelina yuda

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...