KATAVI
Serikali imeombwa kutoa elimu
kwa walimu wa shule za sekondari
wanaotakiwa kuhamishiwa shule za msingi ili kuwandaa kisaikolojia.
Hayo yamebainishwa na mwalimu wa shule ya sekondari mwangaza bi
LILIANI MUGYABUSO wakati akizungumza na mpanda redio kuhusiana na mpango wa
serikali kuwahamisha baadhi ya walimu hao .
Katibu wa chama cha walimu mkoani katavi HAMIS CHINAHOVA amesema
mkakati huo umetokana na wingi wa walimu wa sanaa hivyo kuwapeleka katika shule za msingi kutakuwa na
tija .
Mahitaji ya walimu wa shule
hizo nchini ni laki 2 elfu 35 mia632 ambapo
waliopo ni laki 1 elfu 88 mia 481 hivyo kuwapo kwa upungufu wa walimu elfu 47
mia 151
Chanzo:Ester Baraka
No comments:
Post a Comment