Chama Cha walimu Tanzania CWT Mkoani Katavi kimesema madai
mbalimbali ambayo walimu wanaidai serikali mpaka sasa hayajalipwa.
Hatua hiyo imethibitishwa na Katibu wa chama hicho Mkoani
Katavi Hamis Ismail Chinahova wakati akizungumza na Mpanda radio kuhusu hatua
iliyofikiwa ya kulipwa kwa madeni ya walimu.
Aidha amesema kiasi cha cha shilingi bilioni 1.3 ambacho
walimu Mkoani Katavi wanaidai serikali kinahusu madai ya
likizo,uhamisho,matibabu,masomo na stahiki nyingine muhimu ukiondoa suala la
mishahara.
Kwa mjibu wa taarifa ya iliyokuwa imetolewa na Katibu Mkuu
Wizara ya Fedha na Mipango hivi karibuni,takwimu ya madeni ya watumishi nchini
inaonesha ni zaidi ya shilingi bilioni
127 kati ya hizo walimu wakidai shilingi bilioni 16.25 zilizotakiwa kulipwa
pamoja na mshahara wa mwezi Februari mwaka huu.
Chanzo:Isack Gerlad
No comments:
Post a Comment