MLELE
picha ikionesha wazazi na walezi wakikagua daftari la mwanafunzi (picha na maktaba)
Wazazi mkoani katavi wametakiwa kushirikiana
na walimu pamoja na wadau wa elimu ili kupunguza au kuondoa kabisa idadi ya
wanafunzi wanaohitimu darasa la saba bila kujua kusoma na kuandika.
Hayo yamesema na wadau mabalimbali wa elimu
waliokutana katika kikao kilichofanyika katika Halmashauri ya mlele ili
kutathimini maendeleo ya kielemu katika shule mbalimbali zilizopo mkoani
Katavi.
Wamesema kila mmoja katika jamii ana wajibu
wa kuhakikisha mwanafunzi anajua kusoma na kuandika anapohitimu elimu ya msingi
ili kuboresha elimu nchini.
Kumekuwepo na baadhi ya wazazi ambao hawaonyeshi ushirikiano
katika kuhakikisha mwanafunzi anamaliza elimu ya msingi akiwa anajua kusoma na
kuandika.
Chanzo:Rebbeca kija
No comments:
Post a Comment