Saturday, 17 March 2018

Wanawake wilayani Mpanda wametakiwa kutoa taarifa kuhusu vitendo vya ukatili vinavyofanyika kwenye familia zao.

Picha ya wanawake wa mkoa wa Katavi

MPANDA.
Wanawake wilayani mpanda mkoani katavi  wametakiwa kutoa taarifa  kuhusu vitendo vya ukatili vinavyofanyika kwenye familia zao ili kuweza kukomesha vitendo hivyo.
Akizungumza na mpanda redio Mkuu wa polisi Wilaya ya Mpanda Maria Kwayi amesema,baadhi ya wanawake wamekua wakishindwa kutoa taarifa hali  inayosababisha ongezeko la vitendo vya  ukatili wa kijinsia.
Aidha amesema kuwa wanawake ndio chanzo cha mabadiliko hususani katika kupinga ukatili katika ngazi ya familia na jamii kwa ujumla.
Dawati la jinsia ni kitengo cha polisi kilichoanzishwa mwaka 2007 lengo ikiwa kuhudimia wanawake na watoto kutokana  na kuwepo kwa kesi nyingi za ukatili na unyanyasaji wa kijinsia
Chanzo:Ester Baraka

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...