Wednesday, 7 March 2018

MKUU WA WILAYA YA TANGANYIKA KUWAKAMATA NA KUWAPELEKA MAHAKAMANI WAZAZI WANAOWAZUIA WATOTO WAO KWENDA SHULE.


Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mh. Salehe Mhando Akizungumza na baadhi ya wazazi wa kijiji cha Kamilala kata ya Katuma



TANGANYIKA.

Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi Salehe Mhando amewaagiza viongozi wa kijiji cha Kamilala kata ya Katuma Halmashauri ya wilaya ya mpanda kuwakamata na kuwapeleka mahakamani wazazi wanaowazuia watoto wao kwenda shule.


Akizungumza katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika kijiji hicho Mhando amesema zoezi la kuwakamata wazazi hao limeanza tarehe 5 mwezi huu mpaka tarehe 15 amesema kuna baadhi ya wazazi wamekuwa na tabia ya kuwazuia watoto wao kwenda shule hali ambayo hurudisha nyumba maendeleo ya kitaaluma katika kijiji hicho.

Picha ya Baadhi ya wazazi wa kijiji cha Kamilala kata ya Katuma.


Kwa upande wa mkurugenzi wa wilaya ya Mpanda Rojaz Lumuli amesema jukumu la kuleta maendeleo katika vijiji ni wajibu wa kila mwananchi kwa kushirikiana na viongozi wao katika nyanja mabalimbali.

Kijji cha kamilala kina idadi ya wakazi 1220 ambao wanajihusisha na kilimo na ufugaji shughuli ambazo huwasaidia kuendesha maisha yao ya kila siku.

Chanzo:Paul Mathias

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...