KATAVI.
Baadhi ya
wananchi mkoani katavi wameipongeza mamlaka ya mapato TRA mkoa wa katavi kwa
kutoa elimu juu ya ulipaji wa kodi mbalimbali.
Wakizungumza na mpanda fm kwa nyakati tofauti katika viwanja vya sikonge manispaa ya mpanda
wamesema wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya ulipaji wa kodi kutokana na
kukosa elimu hiyo .
Kwa upande wake
Lazaro Mafiye mtoa elimu kutoka makao makuu TRA
dar es salaam amesema mamlaka
hiyo imeamua kutoa elimu kwa mlipa kodi ili kumuwezesha kulipa kodi kwa hiari
na wakati uliopangwa.
Wiki ya elimu
kwa mlipa kodi inafanyika nchi nzima kuanzia tarehe 5 mpaka 8 march kila mwaka
ikiwa na lengo la kuelimisha, kusikiliza malalamiko, changamoto pamoja na
kupokea mrejesho na maoni mbalimbali kutoka kwa walipakodi.
Chanzo:Ester Baraka
No comments:
Post a Comment