MPANDA.
Wakazi wa kata
ya Nsemulwa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,wameushauri uongozi
wa kata hiyo kupanga vizuri ratiba ya ulinzi shirikishi ili kudhibiti wezi
wanaoiba mali za raia hasa nyakati za usiku.
Wakazi hao kwa
nyakati tofauti wameiambia Mpanda Radio kuwa,uharifu unaotokea kwa sasa katika
mitaa ya kata ya Nsemulwa,hutendeka mapema kabla ya vikundi vya ulinzi kuanza
kulinda.
Aidha,wamezishauri
serikali za mitaa kuhamasisha vikundi vya ulinzi shirikishi katika maeneo yao
kwa kutoa posho,ili kujikimu katika mambo mbalimbali ikiwemo sabuni za
kuwawezesha kufanyia usafi.
Kwa upande wake
diwani wa kata ya Nsemulwa Mh.Bakari Mohamed Kapona,amekiri kuwepo kwa uharifu
mdogo mdogo katani kwake ambapo amesema wanajipanga ili kudhiti uharifu uliopo.
Kata ya Nsemulwa
yenye wakazi wapatao elfu kumi na moja,ni miongoni mwa kata 15 za Halmashauri
ya Manispaa ya Mpanda.
Chanzo:Issack Gerald
No comments:
Post a Comment