Picha ya wananchi wakimwa kwenye mkutano |
MPANDA
Wito umetolewa kwa wananchi wa mkoa wa Katavi manispaa ya
Mpanda kata ya Mwamkulu kuacha tabia ya kufanya mikutano bila kutoa taarifa kwa
viongozi.
Hayo yamesemwa na diwani wa kata hiyo Kalipi Katani wakati
akizungumza na radio mpanda ofisini kwake na kusema kuwa kwa kufanya hivyo
watakiuka utaratibu na watakumbana na sheria ya kupigwa faini maana tarifa hiyo
ilikwisha fikishwa mpaka kwa wananchi.
Diwani katani amesema kuwa kata hiyo inaendeshwa na sheria
tofauti na ilivyokuwa mwanzo kwa kumaanisha kuwa utolewaji wa faini hizo ndio
chanzo cha mapato katika kata.
Pia amewaasa wananchi wote wanaofanya mikutano ambao si
viongozi hairuhusiwi na kuwataka viongozi wote kufuata taratibu za vibali na
taarifa kwa viongozi husika kabla ya kufanya mikutano.
Chanzo:Ezelina Yuda
No comments:
Post a Comment