MPANDA
Katika
kuelekea siku ya elimu ya mlipa kodi
Tanzania wananchi wa Mkoani katavi
wametakiwa kujitokeza kwa wingi ili kupata elimu juu ya ulipaji kodi.
Hayo
yamesemwa na meneja wa TRA mkoa wa
katavi Enos Magimba wakati akizungumza kwa njia ya simu na mpanda radio na
kusema kuwa ni muhimu kwa watanzania kupata elimu ya ulipaji kodi hususan
wafanya biashara.
Magimba
amesema kuwa utoaji wa elimuya mlipa kodi
mkoani katavi unafanyika kuanzia Nyanja zote za kimkoa mpaka vijijini na
kuwataka wananchi kutosubiri wakati wa maadhimisho pekee.
Siku ya mlipa kodi mkoani Tanzania ili zinduliwa na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi
Richard Kayombo kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),ambapo hufanyika kuanzia tarehe 5 mpaka 8
march kila mwaka ikiwa na lengo la
kuelimisha, kusikiliza malalamiko, changamoto pamoja na kupokea mrejesho na
maoni mbalimbali kutoka kwa walipakodi.
Chanzo:Ezelina Yuda
No comments:
Post a Comment