MPANDA
Mkazi wa kata ya Misungumilo Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda
anayefahamika kwa jina la Mohamedi Futakamba (40) amefikishwa mahakamani kwa
kosa la wizi wa kuaminiwa.
Tukio hilo limetokea tarehe 19 mwezi wa pili saa 6 mchana katika maeneo ya soko kuu
mtuhumiwa ambaye ni fundi uchomeleaji alimwibia bwana Martin Lucas nondo 9
zenye thamani ya shilingi 126,000 ambazo zilikuwa kwa ajili ya ukarabati wa
madirisha.
Kesi hiyo imesikilizwa katika Mahakama ya mwanzo mbele ya hakimu
Elisante Paranjo na mwendesha mashtaka wa jeshi la polisi WP.Mwanaidi Nasoro na
mshitakiwa kukana kutenda kosa hilo.
Hata hivyo kesi hiyo imeahirishwa mpaka tarehe 8 mwezi huu
itakaposikilizwa tena na mtuhumiwa amerudishwa rumande.
Kutenda kosa la wizi ni kinyume na kifungu cha 265 cha sheria sura ya
16 kama ilivyofanyiwa mabadiliko mwaka 2016.
Chanzo:Furaha Kimondo
No comments:
Post a Comment