KATAVI
Mkoa wa Katavi umetajwa kuporomoka kitaaluma katika ufaulu wa
wanafunzi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo utoro wa wanafunzi shuleni
pamoja na uhaba wa walimu.
Hatua hiyo imebainishwa na Afisa elimu taaluma mkoani Katavi Mwalimu
Nyalinga katika semina ya siku mbili kwa waandishi wa habari ili kuwawezesha
wandishi hao kuripoti kwa weledi miradi ya elimu.
Afisa Elimu Taaluma Mkoani Katavi anayeshughulikia Elimu ya watu
wazima Mwalimu John Pandisha aliyekuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Afisa elimu
Mkoa,amesema Equip Tanzania inasaidia mambo mbalimbali ikiwemo kuboresha
majengo ya shule na usimamizi wa elimu kwa ujumla.
Mkoa wa Katavi mwaka 2014,2015 na 2016 ulikuwa ukishika nafasi ya
kwanza kitaifa katika mtihani wa darasa la saba ambapo kwa mwaka 2017 ufaulu
umeshuka mpaka nafasi ya tisa kitaifa.
Source:Issack
No comments:
Post a Comment