Monday, 5 March 2018

WANANCHI WA KIJIJI CHA ITETEMYA KATA YA KALEMA WAMEIOMBA SERIKALI KUWASAIDIA KUBORESHA MIUNDOMBINU.



 TANGANYIKA

Wananchi wa kijiji cha Itetemya kata ya kalema wilaya ya Tanganyika wameiomba serikali kuwasaidia kuboresha miundombinu ya barabara na madaraja kwani wanashindwa kufanya shughuli za maendeleo hususani kipindi cha mvua za masika.

Hayo yamesemwa na baadhi ya wananchi wa kijiji hicho katika ziara ya Mbunge wa Mpanda vijijini Seleman Kakoso na kusema kuwa mbali na ubovu wa miundombinu kukwamisha shughuli mbalimbali pia wanafunzi wamekuwa wakikosa masomo baada ya daraja kujaa maji.

Kwa upande wake Mbunge wa Mpanda vijijini amesema kuwa tayari serikali imetoa fedha za dharula kwa wakala wa barabara za mijini na vijijini Tarula  kwaajili ya kurekebisha barabara hizo.

Licha ya kuanzishwa kwa wakala barabara za mijini na vijijini bado kikwazo cha miundombinu kinaathiri maendeleo ya uchumi  hususani katika maeneo ya vijijini.

Chanzo:Restuta Nyondo

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...