Baadhi ya wananchi katika halmashauri ya
Manispaa ya Mpanda wamelishauri jeshi la Polisi Mkoani Katavi,kuongeza kasi ya
kuwa karibu na wananchi ili kudhibiti uharifu mbalimbali unaoendelea kutokea
mkoani hapa.
Ushauri huo umetolewa na wananchi hao
kwa nyakati tofauti,wakati wakizungumza na Mpanda Radio kuhusu mwenendo wa hali
ya usalama ilivyo kwa sasa katika maeneo mbalimbali ya Mkoa.
Kwa upande wake diwani wa kata ya
Nsemulwa Mh.Bakari Mohamed Kapona amesema,matukio ya mauaji yanayotokea
yanatakiwa kuwa funzo kwa jeshi la polisi na watanzania kushikamana pamoja ili
kupambana na uharifu unaotokea.
Jeshi la Polisi Mkoani Katavi limekuwa
likitoa wito kwa wananchi kuripoti mapema matukio au viashiria vya uharifu ili
vidhibitiwe kabla ya kusababisha madhara.
Katika kipindi cha miezi miwili
iliyopita,watu watatu wamepoteza maisha na wengine zaidi ya watano kujeruhiwa
katika matukio mbalimbali kutokana waharifu kuvamia wananchi Mkoani Katavi.
Chanzo:Issack Gerald
No comments:
Post a Comment