Monday, 5 March 2018

HOSPITALI YA WILAYA YA MLELE IMEKIRI KUKABILIWA NA UHABA WA VIFAA TIBA KATIKA CHUMBA CHA UPASUAJI.


Picha ya hospitali ya wilaya ya Mlele


MLELE

HOSPITALI YA WILAYA YA MLELE ILIYOPO TARAFA YA INYONGA MKOANI HAPA IMEKIRI KUKABILIWA NA UHABA WA VIFAA TIBA KATIKA CHUMBA CHA UPASUAJI HALI INAYOLAZIMU BAADHI YA WAGONJWA KUSAFIRI UMBALI WA KILOMITA 200 KWENDA KUTAFUTA HUDUMA ZA UPASUAJI

AKIONGEA HOSPITALINI HAPO MGANGA MKUU WA WILAYA YA MLELE DR.LUCIA KAFUMU AMEBAINISHA KUWEPO KWA CHANGAMOTO HIYO LICHA YA KUANZA KUTOA HUDUMA YA UPASUAJI INAYOSAIDIA KUOKOA MAISHA YA WATU.

KWA UPANDE WAKE MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA KATAVI MHE.ANNA RICHARD LUPEMBE (CCM) AMETEMBELEA HOSPITALINI HAPO NA KUSHIRIKI ZOEZI LA USAFI AMBAPO AMEKABIDHI VIFAA TIBA KWA AJILI YA KUPIMA WINGI WA DAMU VYENYE THAMANI YA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 9 NA KUAHIDI KUTATUA CHANGAMOTO ILIYOPO.

BAADHI YA WAGONJWA HOSPITALINI HAPO WAKAELEZA KUPATA HUDUMA ZINAZOSTAHILI LICHA YA KUWEPO KWA CHANGAMOTO YA WAHUDUMU WACHACHE KULINGANA NA UHITAJI WA HOSPITALI.

CHANZO:EDWARD MGANGA


No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...