Monday, 5 March 2018

WAKAZI WA KITONGOJI CHA LUHAFWE KATA YA TONGWE WANALAZIMIKA KUTEMBEA ZAIDI YA KILOMITA 20 KUFUATA HUDUMA YA AFYA KATIKA VIJIJI JIRANI.


Picha ya kituo cha huduma ya afya


TANGANYIKA

Wakazi wa kitongoji cha Luhafwe kata ya Tongwe iliyopo wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi wanalazimika kutembea zaidi ya kilomita 20 kufuata huduma ya afya katika vijiji jirani.

Wakizungumza na Mpanda radio wakazi hao wamsema wanalazimika kuhudumiwa na zahanati ya Kijiji cha Vikonge ambayo iko mbali kitendo kinachohatarisha maisha yao hasa akina mama wajawazito kwani wengi wao hujifungulia nyumbani.

Wameongeza kuwa siku za nyuma wakazi wa kitongoji  cha Luhafwe serikali iliwachukulia kuwa ni wavamizi hivyo haikuona umuhimu wa kuwapelekea huduma za kijamii

Mwenyekiti wa kitongoji hicho bwana Malaika Bujiku amesema baada ya serikali ya wilaya kukirasimisha kitongoji hicho kuwa makazi rasmi tayari wameshalifikisha suala hilo katika ngazi ya wilaya na kuahidi kupekelekewa huduma ya afya japo utekelezaji wake unaonekana kutopewa kipaumbele.

Chanzo:Haruna Juma 


No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...