TANGANYIKA
Wakazi katika kitongoji
cha Luhafwe kata ya Tongwe wilayani Tanganyika Mkoani Katavi, Wako hatarini
kukumbwa na magonjwa ya milipuko kuokana na maji wanayotumia kutokuwa safi na
salama.
Wakazi
hao wameiambia Mpanda Radio kuwa,chanzo cha maji wanachokitegemea wanatumia na
mifugo,na shughuli za kilimo hivyo
huhofia matatizo kwa afya zao kutokana na kukosa chanzo kingine kinachoweza kuwapatia maji.
Naye mwenyekiti wa kitongoji hicho Bw.Malaika
Bujiku na katibu wake Paul Nkingwa Mabenga wamemtupia lawama mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Muhando sanjari
na kuoneshwa kero hiyo lakini mpaka sasa hakuna hatua iliyochukuliwa na
serikali ili kuwanusuru wananchi na hali hiyo.
Sanjari
na mwaka 2016,serikali ya wilaya hiyo kupitisha azimio la kujenga mji wa
kibiashara katika eneo la Luhafwe mpaka sasa imebainishwa kuwa hakuna huduma za kijamii ikiwemo shule,afya na maji
bado ziko duni.
Chanzo: Issack Gerald
No comments:
Post a Comment