MPANDA
Wananchi wilayani mpanda
mkoani katavi wameshauriwa kufika hospitali mara moja pale wanapogundua kuwa na
matatizo ya kinywa na meno.
Akizungumza na mpanda fm ofisini kwake daktari wa magonjwa ya kinywa
na meno wiliam lwesia katika hospitali ya manspaa ya mpanda Amesema kuwa magonjwa hayo hayasababishwi na
imani za kishirikana ila ni viini vya
magonjwa vitokanavyo na baktria na mabaki ya magonjwa .
Hata hivyo Dokta Lwesia amebainisha
moja ya njia ya kujikinga na magonjwa ya kinywa na meno ni kuzingatia suafi wa
kinywa na meno kwa kupiga mswaki walau mara mbili kwa siku asubuhi na jioni na Kudhibiti
na kupunguza ulaji wa vyakula vyenye sukari kwa wingi itakuepusha na magonjwa
ya kinywa na meno.
Chanzo:Ester Baraka
No comments:
Post a Comment