KATAVI
Wanawake mkoani katavi
wametakiwa kuadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kutetea haki zao za msingi.
Hayo yamesemwa na afisa
maendeleo ya jamii mkoani katavi Bi,Anna shumbi na kubanisha kuwa katika siku hii ya wanawake
ili kuwakutanisha wanawake kuweza
kutafakari mambo yanayowahusu katika kujikwamua katika Nyanja mbali mbali za
kiuchumi.kijamii na kimaendeleo.
Aidha Shumbi amesema kuwa
wanawake wamepiga hatua katika swala zima la maendeleo kama vile kielimu,
kimaisha na kifamilia.
Siku ya wanawake dunian inayo
adhimisha tarehe 8 March kila mwaka kitaifa
inabebwa na kauli mbiu inayosema kuelekea uchumi wa viwanda
tuimarishe uchumi wa jinsia na uwezeshaji wanawake vijijini ambapo mgeni
rasmi anatarajiwa kuwa mkuu wa mkoa wa
KataviMstaafu Meja Jenerali Rapahaeli Muhuga
Chanzo:Ezelina Yuda
No comments:
Post a Comment