MPANDA.
Walimu wakuu wa shule mbalimbali katika halmashauri
ya manispaa Mpanda Mkoani Katavi wameushukuru mradi wa SSRP wenye lengo la
kuboresha viwango vya elimu kwa upande wa watoto wa kike kuwatembelea katika
shule zao kutawapa chachu ya kuwasaidia watoto wa kike wafikie malengo yao.
Wameyasema
hayo walipozungumza na mpanda radio na kusema kuwa kuepo kwa mradi huo
kutawasaidia ikiwa nipamoja na jamii kutambua umuhimu wa mtoto wa kike katika
jamii napia utasaidia kupunguza mimba za utotoni.
Kwa upande
wao walimu ambao wamekuwa wakitoa elimu hiyo wamesema kuwa mafunzo yameenda
vizuri na umewasaidia wasichana wengi kufaulu vizuri na kueleza changamoto
ilitokana na wazazi wengi kutoyaamini mafunzo hayo.
Mradi wa
SSRP ni mradi ambao nimkakati wa kuinua elimu kwa watoto wa kike na kuwaepusha
watoto kutofikia malengo kwa kujikinga na vikwazo ambayo vinawsababisha wapate
mimba na kutoendelea na masomoyao.
Chanzo:Revocatus
Msafiri
No comments:
Post a Comment