Thursday, 8 March 2018

MKUU WA MKOA WA KATAVI AMEWATAKA WANAUME KUSHIRIKIANA NA WANAWAKE KATIKA VITA DHIDI YA UMASIKINI.

Mkuu wa mkoa wa katavi Meja Jenereali Mstaafu Rafael Muhuga


TANGANYIKA.
Mkuu wa mkoa wa katavi Meja Jenereali Mstaafu Rafael Muhuga amewataka wanaume kushirikiana na wanawake katika vita dhidi ya umasikini.

Kauli hiyo ameitoa katika kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake iliyofanyika kimkoa katika kata ya sibwesa wilayan Tanganyika mkoani Katavi Katika hotuba yake Muhuga amesema endapo jamii ikishirikiana kwa pamoja vita hiyo itakuwa imekwisha ndan ya jamii.

Awali akisoma risala mwenyekiti wa jukwaa la wanawake wilayan Tanganyika Helen kipoki amesema kuwa wanawake kwa pamoja wamejipanga kupambana na umasikin kwa vitendo baada ya kutekeleza Sera ya Tanzania ya viwanda.

Nao baadhi ya wajasiriamali  wanawake waliohudhuria sherehe hizo wamesema kuwa wameiomba serikali kuiwasaidia upatikanaji wa soko ili kurahisisha uuzwaji wa bidhaa wanazozalisha.

Siku ya mwanamke inayofanyika kila March 8 ya kila mwaka ambapo  kitaifa iliyofanyika mkoani mbeya imebebwa na kauli mbiu kuelekea uchumi wa viwanda tuimarishe usawa wa jinsia na uwezeshaji wa wanawake vijijini.

Chanzo: Edward Mganga

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...