MPANDA
Wanawake wa Halmashauri
ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamewataka wanaume kutenda haki kwa
kuzingatia usawa.
Wameyasema hayo kwa
nyakati tofauti wakati wakizungumza na mpanda radio katika soko la buzogwe na
kusema kuwa wanaume wengi hawawapatii wanawake wengi fursa kutokana na mfumo
dume kutumika katika familia nyingi.
Kwa upande wao wanaume
wamekuwa na mitazamo tofauti huku wakisema kuwa usawa wa wanawake umepitiliza
na wengine kusema asilimia hizo zipunguzwe kwa kuogopa kudharauliwa.
Siku ya wanawake duniani
huazimishwa kila tarehe 8 machi ya kila
mwaka na kauli mbiu ya mwaka huu ni”KUELEKEA UCHUMI WA VIWANDA TUIMARISHE USAWA
WA KIJINSIA NA UWEZESHAJI WANAWAKE VIJIJINI”na
Mkoani Katavi maadhimisho ya siku ya wanawake yamefanyika katika kata ya sibwesa iliyoko katika Wilaya
ya Tanganyika.
Chanzo:Furaha
Kimondo
No comments:
Post a Comment