Picha na kibao cha shule msingi Nsanda |
Zaidi ya Wanafunzi 390 wa shule ya Msingi Nsanda
katika kijiji cha Nsanda Kata ya Kanoge
halmashauri Ya Nsimbo Mkoani Katavi wamekatishwa masomo kutokana na
nyumba za wakazi kijijini hapo kuchomwa
Moto kwa madai ya kuwa katika hifadhi ya misitu.
Mpanda redio imezungumza na baadhi
ya waliokua wananfunzi wa shule hiyo na miongoni mwao wanatarajia kufanya
mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi ambapo kwa sasa wanasintofahamu ni wapi
watapata elimu.
Insert…..Wanafunzi.
Kwa upande wake aliyekua mwenyekiti
wa kijiji hicho cha Nsanda Bw. Minani Vizabigomba amesema kwamba wanaskitishwa
na kitendo cha kuchomwa kwa makazi ya
kijiji hicho ambacho amedai kina usajili halali.
Shule hiyo imejengwa kwa ufadhiri wa
serikali ya watu wa uingereza, shirika
la kuhudumia wakimbizi UNHCR kwa
kushirikiana na serikali ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment