Monday, 28 August 2017

Wananchi mkoani katavi wametakiwa kuzingatia usafi na kutumia maji safi na salama.






Wananchi mkoani katavi wametakiwa kuzingatia usafi na kutumia maji safi na salama ili kujikinga na magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu.
Hayo amebainishwa na kaimu mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya mpanda Dr Seleman Mtenjela wakati akitolea ufafanuzi kuhusiana na ugonjwa wa kipindupindi ambao unasababishwa na kutozingatia kanuni za usafi.

Dr Selemani amesema jamii lazima ijifunze kutumia maji safi na salama pamoja na kunawa mikono kwa maji na sabuni mara baada ya kutosha chooni ili kuua vijidudu vya magonjwa yanayosababishwa na kutozingatia usafi.

Aidha ameeleza kuwa kata ya Ikola ,Isengula na kalema zinaathirika zaidi kutokana na muungiliano wa watu kutoka katika maeneo yanayozungukwa na ziwa Tanganyika.

Kwa upande wa Afisa habari wa wilaya yam panda Syvanus Ntiyakenya amewataka wananchi kuzingatia swala la usafi na kutumia vyoo vilivyobora ili kukomesha magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu.

Usafi ukizingatiwa na kila mmoja magonjwa yanayosababishwa na uchafu yanaweza kutokomezwa.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...