Monday, 28 August 2017

Mkoa wa katavi kwa sasa upo katika Mpango wa kuangalia Zao lingine la biashara ili kuleta maendeleo.

Mkuu wa Mkoa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Mugoya Muhuga













Mkoa wa katavi kwa sasa upo katika Mpango wa kuangalia Zao lingine la biashara ili kuleta maendeleo katika mkoa huo.
Hayo yamsemwa na Mkuu wa Mkoa wa katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga ijumaa hii katika   kikao maalum cha baraza la Madiwani wa halmashauri ya manispaa ya Mpanda cha kujadili hoja za utekelezaji wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2015/16.
Amesema tayari amefanya mawasiliano na Mkurugenzi wa bodi ya korosho kutoka mtwara ambao wanajiandaa kuja mkoani katavi kwa ajili ya kuangalia maeneo kuona kama zao la korosho linaweza kuwa moja ya Mazao hapa Mkoani.

Aidha amesema kuwa hatua hiyo ni baada ya  kuona zao la tumbaku ambayo ilikua inaleta asilimia 60 ya mapato katika halmashauri za Mkoani katavi kuonekana halina uhakika. 

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...