Thursday, 23 November 2017

Mahakama ya wilaya ya Mlele imemhukumu kwenda jela diwani wa kata ya Katumba Senator Baraka



 

 Na Haruna Juma.

Mahakama ya wilaya ya Mlele imemhukumu kwenda jela diwani wa kata ya Katumba Senator  Baraka kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa.

Mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo Timothy Swai, mwendesha mashtaka wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa katavi Bahati Haule amedai kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo 12.05.2016.

 Amesema mtuhumiwa huyo aliomba rushwa ya sh. laki 5 ili asimuhamishe mfugaji mmoja kwenye eneo lilozuiliwa na mahakama kuendesha shughuli za ufugaji.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa kosa la kuomba rushwa mtuhumiwa amehukumiwa kutoa faini ya sh. laki 5 au kifungo cha miaka mitatu na kosa la kupokea rushwa mtuhumiwa amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...