Thursday, 23 November 2017

Serikali ya manispaa ya Mpanda mkoani Katavi imesema imejipanga kuboresha miundombinu ya vyumba vya madarasa kwa shule za sekondari




Na Safina Joel

Serikali ya manispaa ya Mpanda mkoani Katavi imesema imejipanga kuboresha miundombinu ya vyumba vya madarasa kwa shule za sekondari ili kuwawezesha wanafunzi wote watakaochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani. 

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa manispaa ya Mpanda Maiko Nzyungu wakati akizungumza na Mpanda Radio, na kusema kuwa miongoni mwa mipango iliyopo ni kuhakikisha kuwa kata zote ambazo hazikuwa na sekondari.

Kauli ya Nzyungu imekuja ikiwa ni siku Chache baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani  Jafo kuagiza kuanza mapema maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2018, kufuatia kuongezeka kwa ufaulu.


No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...