Thursday, 23 November 2017

Aliyewahi kuwa Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila amejivua uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).




Aliyewahi kuwa Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila amejivua uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Kafulila Amefanya hivyo kwa kile alichodai kuwa hana imani tena na upinzani, kama jukwaa salama la kupambana na ufisadi.

Amesema kuwa vyama vya upinzani nchini vimepigwa ganzi na kupooza ghafla katika harakati zake za kupambana na ufisadi, baada ya Rais Dk John Magufuli kuendesha vita hiyo kwa mafanikio makubwa.

Ameongeza kuwa  mafanikio hayo ya Rais Magufuli, yameufanya upinzani kuwa siyo jukwaa salama tena katika vita dhidi ya ufisadi; na ndiyo maana kwa hiari na utashi wake, ameamua kujivua uanachama wa Chadema.

SOURCES:HABARI LEO.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...