Wakizungumza mara baada ya kutangazwa washindi wameushukuru uongozi wa Mpanda radio kwa kuona umuhimu wa suala hilo na kwamba itaongeza ufanisi wa kazi miongoni mwao, ili kujenga tasinia ya habari yenye tija kwa jamii.
Kwa upande wa meneja Mkuu wa Mpanda radio fm Bw Revocuts Endru amesema nia ya kuwatangaza wafanyakazi bora kwa kila mwezi ni kuchochea uwajibikaji kwa kila mfanyakazi na kwamba zoezi hilo ni endelevu kwa kila mwezi.
Awali uongozi wa mpanda radio fm ulipendekeza majina manne ambayo yamepigiwa kura ya wazi na wafanyakazi wote na watatu kati yao kupata kura sawa.
Washindi hao ni Salome Mchawa ambaye ni Mhasibu, Safina Joel mwandishi wa habari na Mtangazaji na Denis Mkakala ambaye ni Mwandishi wa habari, na mtangazaji huku akihudumu nafasi ya afisa masoko.
Meneja wa mpanda fm radio amesema kwamba kutakuwa na uchaguzi wa mfanya kazi bora wa mwezi ili kuongeza kasi na maendeleo ya kituo chetu pia na kuongeza ufanisi wa wawafanyakazi wa kituo cha mpanda fm.
No comments:
Post a Comment