Mahakama ya Juu nchini Kenya imefuta ushindi wa rais Uhuru Kenyatta katika Uchaguzi uliofanyika tarehe 8 mwezi uliopita.
Uamuzi huo ulitangazwa na Jaji Mkuu David Maraga jijini Nairobi Ijumaa asubuhi.
Jaji Maranga alisema kuwa kati ya Majaji sita waliosikiliza kesi hiyo, wanne walifikia uamuzi kuwa Uchaguzi huo haukufanyika kwa mujibu wa Katiba ya sheria za Uchaguzi nchini humo.
Aidha, wamesema kuwa kulikuwa na udanganyifu mkubwa sana katika Uchaguzi huo na hivyo haukuwa huru na haki.
“Tumebaini kuwa, Uchaguzi huu haikuwa huru na haki na hivyo, mshindi aliyetangazwa hakupata ushindi,” alisema Maraga.
Hatua hii ya Mahakama ya Juu inamaanisha kuwa, Uchaguzi Mkuu mpya utafanyika tena baada ya siku 60 kwa mujibu wa Katiba ya nchi hiyo.
Uamuzi huu umeleta furaha kwa wafuasi wa muungano wa upinzani NASA, waliokuwa wanasubiri uamuzi huu kwa hamu kubwa.
Wakili wa rais Uhuru Kenyatta, Abdulnasiir Muhammed amepinga uamuzi wa Mahakama na kusema kuwa, ulikuwa ni uamuzi wa kisiasa uliofikiwa.
No comments:
Post a Comment