Thursday, 31 August 2017

Mtu mmoja amelazwa katika hospital baada ya kujeruhiwa na simba katika kata ya mtapenda mkoani katavi .



MPANDA
Mtu mmoja amelazwa katika hospital ya manispaa ya Mpanda baada ya kujeruhiwa na simba katika kata ya mtapenda mkoani katavi .
Akithibitisha k mganga mkuu wa hospital ya manispaa ya Mpanda Dr Theopister Elisa amesema amempokea majeruhi huyo mwenye umri wa miaka kumi na tano na anaendelea kupatiwa matibabu zaidi.

Kwa upande wa diwani wa kata ya mtapendwa Fyula Samwel amesema kuwa simba wapo watatu ambao wanazunguka katika maeneo ya kata hiyo na yameshaua mbuzi 8 na ng’ombe 7 na kumjeruhi mtu mmoja.

Hata hivyo Bwana Fyula amewataka wananchi wasiende maeneo ya porini mtu mmoja na kuacha kutembea wakati wa usiku  mpaka hali itakapo kuwa nzuri.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...