Thursday, 31 August 2017

Richard Mbogo amewataka wananchi walioondolewa katika kata ya starike mkoani katavi kuwa wavumili wakati taratibu zinafanyika kurudishwa katika maeneo yao .


MPANDA
Mbunge wa Nsimbo Mh. Richard Mbogo
Mbunge wa jimbo la Nsimbo  mkoani katavi Mh. Richard Mbogo amewataka wananchi walioondolewa katika kata ya starike mkoani katavi kuwa wavumili wakati taratibu zinafanyika ili waweze kurudishwa katika maeneo yao .

Ameyasema hayo wakati akizungumza na Mpanda redio kasema kuwa wananchi wa mgorokani wameondolewa kimakosa katika maeneo  yao na hivyo taratibu zinafanyika ili waweze kurejeshwa kwani walikuwa kisheria.

Hata hivyo amesema taratibu zitakapomalizika watarudishwa na kuendelea na shughuli zao walizokuwa wanazifanya kabla ya kuondolewa kama vile kilimo.


Hivi karibuni operesheni ya kuwaondoa wananchi katika maeneo yanayosemekana kuwa ni miliki ya hifadhi mkoani katavi imekumba maeneo mengi ikiwemo Mgolokani ,makutanio na Litapunga na Luhafwe.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...