Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Abdalah Malela amemvua madaraka Mwalimu Mkuu
Masunga Ng’waya wa Shule ya Msingi Mwashagata, iliyopo kijiji hicho kata ya
Ihusi kwa kosa la ukosefu wa maadili.
Akizungumza jana, mkurugenzi huyo amesema tukio hilo limetokea hivi karibuni baada ya mwalimu mmoja wa shule yake kumrubuni mwanafunzi wake kwa kufanya mapenzi naye tena kwenye nyumba yake, kitendo ambacho ni cha kukosa maadili.
Aidha, amesema kesi hiyo tayari imefikishwa polisi na wakati wowote mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani.
SOURCES:HABARI LEO.
No comments:
Post a Comment