Tuesday, 2 January 2018

Serikali imeongeza muda wa miaka miwili ya umiliki wa leseni za vitalu 95 vya uwindaji wa kitalii ambazo muda wake umeisha.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla 

DODOMA

Serikali imeongeza muda wa miaka miwili ya umiliki wa leseni za vitalu 95 vya uwindaji wa kitalii ambazo muda wake umeisha.
Uamuzi huo umetolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla wakati wa kikao cha majumuisho na watendaji wa Wizara hiyo muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano wa wadau wa sekta hiyo ulioandaliwa na Wizara hiyo mjini Dodoma.
Akizungumzia uamuzi huo amesema, lengo ni kuwapa muda wawekezaji hao ili waweze kujiandaa na mabadiliko ya mfumo mpya wa utowaji wa leseni za vitalu vya uwindaji wa kitalii kwa njia ya mnada ikiwemo kurudisha baadhi ya gharama za uwekezaji.

Katika hatua nyingine amesema mnada huo utaanza siku za mwanzo wa mwezi huu.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...