Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk. Mwigulu Nchemba |
RUVUMA
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dk.
Mwigulu Nchemba amewataka wananchi kujiandikisha kupata kitambulisho cha Taifa
kwani si zoezi la hiari ni lazima kwa kila Mtanzania aliyeko ndani ya mipaka ya
nchi ili kutambuliwa.
Amesema hayo akizindua zoezi la
kujiandikisha kupata kitambulisho cha Taifa na kugawa vitambulisho katika
mkoa wa Ruvuma na kukagua zoezi hilo linaendaje kwa mikoa ya nyanda za kusini
hasa iliyoko mipakani mwa nchi.
Waziri mwigulu amewataka wananchi
waache mazoea ya kutafuta kutambuliwa mpaka wanapokuwa na shida hasa za kutaka
hati ya kusafiria au migogoro ya ardhi pale anapoambiwa yeye si raia wa
Tanzania.
Naye Kaimu Mkurugenzi mkuu wa
vitambulisho vya Taifa Andrew masawe amesema zoezi la kuandikisha wananchi
linatakiwa kuisha ifikapo mwezi December 2018 huku akitaja changamoto
wanazokutana nazo kuwa ni la viambatanisho vile vinavyoonyesha umli wa mtu na
makazi kwani wananchi huwa hawaendi navyo wakat wa kujiandikisha.
SOURCE:MOO BLOG
No comments:
Post a Comment