SHINYANGA
Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Joseph Dogani (50) mkazi wa
kata ya Ndala Mjini Shinyanga anayedaiwa kuwa ni jambazi ameuawa kwa kupigwa
risasi na polisi sehemu mbalimbali za mwili wake akidaiwa kutaka kuwapiga
risasi askari polisi.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa polisi mkoa wa
Shinyanga ACP Simon Haule amesema tukio hilo limetokea Januari 1,2018 saa 9:45
alasiri.
Amesema Joseph Dogani alifariki papo hapo baada ya kupigwa
risasi na polisi baada ya marehemu kutaka kuwapiga risasi askari waliokuwa
wanamfuatilia.
Kamanda Haule amesema baada ya kupekuliwa alikuwa na bastola
yenye risasi nne ndani ya magazine.
No comments:
Post a Comment