MPANDA
Baadhi
ya wananchi Mkoani Katavi wameeleza kuwa
endapo sera ya viwanda ikitekelezwa kwa vitendo itapunguza Wimbi la ukosefu wa
ajira.
Kauli
hiyo inajiri ikiwa ni siku chache baada ya kuzinduliwa kwa sera ya Tanzania
mpya ya viwanda iliyofanyika mkoani Dodoma iliyokwenda samba mba na tamko la
serikali kuwa kila mkoa uwe umejenga
viwanda 100.
Aida
wameongeza kwa kusema kuwa ni vema watu wote kujishughulisha ili kuweza kufikia
uchumi wa viwanda sanjari na kusaidia watu wengi ambao walikosa ajira na kuwepo
mitaani kupata fursa ya kuweza kujishughulisha.
Waziri Nchi,ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
serikali za mitaa(Tamisemi) Seleman Jafo
alitoa tamko kwa wakuu wa mikoa wote kuwa
disemba mwaka huu hadi mwakani mikoa yote 26 ya Tanzania bara inapaswa
kujenga viwanda 100
Source Ester,
No comments:
Post a Comment