MPANDA
Mwenyekiti wa bonde la mto Mpanda Bw. Mikidadi Marubaro Mbuganzito amewataka wakazi wote waishio
kando na mto huo, kutii sheria ya kutofanya shughuli zozote za kibinadamu ndani ya mita 60 kutoka katika
kingo za mto.
Pamoja na mambo mengine Bw.Mikidadi Mbuganzito amesema agizo la rais kuhusu shughuli za kibinadamu kama kilimo kufanyika kandokando ya mto lilihusu eneo la Kagera pekee na siyo mito yote nchini.
Kauli hiyo imekuja baada ya mkulima mmoja Bundala
Sweya wa kijiji cha Itenka B kudai kukamatwa na kudaiwa faini ya shilingi laki
mbili baada ya kulima kando ya mto huo akidai kutekeleza agizo la rais wa Jamhuri
ya muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli.
Kwa upande wake diwani wa kata ya itenka Joseph
Laurent amewataka wananchi kushirikiana na serikali ili kama kuna mambo
hayaendi sawa wawataarifu viongozi husika ili wasaidiwe.
Novemba
7 mwaka huu rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli
akiwa Kyaka mkoani kagera alisema mamlaka zinazosimamia mazingira yafaa
ziangalie namna ya kutekeleza sheria ya mazingira nchini
Source Haruna juma.
No comments:
Post a Comment