Saturday, 18 November 2017

Viongozi wa dini Mkoani Katavi wameaswa kutumia taaluma na karama zao katika kuunganisha jamii inayomtambua mungu mionyoni mwao na kuhimiza waumnini kutotenda matukio yanayoleta athari kwa jamii hapa nchini.


NSIMBO
Viongozi wa dini Mkoani Katavi wameaswa kutumia taaluma na karama zao katika kuunganisha jamii inayomtambua mungu mionyoni mwao na kuhimiza waumnini kutotenda matukio yanayoleta athari kwa jamii hapa nchini.

Wito huo umetolewa jana na Mchungaji Zacharia Andrea kutoka chuo cha Biblia Bigabilo kilichopo mkoani Kigoma,aliyekuwa mgeni rasmi katika mahafali ya kuhitimu wanafunzi wa shule ya biblia FPCT Katumba yaliyofanyika Misheni ya Katumba akisema viongozi wanatakiwa kuwa mfano wa kuigwa kwa matendo mema.

Kwa upande wake Mkuu wa shule ya biblia FPCT Katumba Mchungaji Elisha Musenda,katika taarifa yake amesema,shule ya biblia FPCT Katumba,imesaidia kupatikana viongozi wazuri wa kanisa wanaoshirikiana na jamii katika kuleta maendeleo hapa nchini.
Katika risala ya wanafunzi ambayo imesomwa na mwinjilisti  Moris Samson,wameomba mafunzo yawe endelevu katika shule hiyo huku Mchungaji kiongozi wa kanisa la FPCT Katumba Mchungaji Wilium Isaya  akisema kuendelea kwa mafunzo katika shule hiyo ni maamuzi ya kanisa ngazi ya taifa.

Jumla ya wanafunzi 15 wa shule ya biblia FPCT Katumba wamehitimu elimu ya mwaka mmoja wa ngazi ya cheti kwa mwaka 2017 na kufanya kuwa mahafali ya 13 tangu miaka ya 1990 yalipoanza kwa mara ya kwanza.
Source Issack Gerald

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...