Picha ya wadau wa salaam wakiwa katika ziara ya kutembelea kituo cha mpanada Radio Fm |
MPANDA
Wadau wa salaamu kupitia vyombo vya
habari Mkoani Katavi,wameaswa kushiriki kwa kiasi kikubwa kuibua masuala
mbalimbali ya kijamii ikiwemo kuibua matukio yanayoiathiri jamii ikiwemo
matukio ya ukatiri.
Wito huo umetolewa leo na Meneja wa
kituo cha Mpanda Radio Bw. Revocatus Msafiri,wakati akizungumza na viongozi wa
vikundi vya wanasalaamu kuanzia ngazi ya kata hadi Mkoa kikao ambacho kimefanyika
katika ukumbi wa studio ya Mpanda Radio.
Picha ya wafanyakazi wa mpanda radio wwakiwa na wadau wa salaam |
Katika hatua nyingine, Bw. Msafiri
amesema bonanza la leo la mchezo wa mpira wa miguu baina ya watumishi Mpanda
Radio na watuma salaamu Mkoani Katavi linalenga kupanua wigo wa kufahamiana na kuongeza
mahusiano yenye tija kwa jamii.
Kwa upande wao baadhi ya watuma
salaamu,akiwemo mwenyekiti watuma salaamu wilayani Mpanda Edimond John na Mkuu
wa nidhamu Bw.Sospeter Mzee wa Tai mbali na kuipongeza Mpanda Radio kwa matangazo
yanayozingatia mahitaji ya jamii,pia wameiomba
Mpanda Radio kuwafikia wananchi waishio vijijini kutokana na vyombo vya habari
kutofika mara kwa mara.
Watuma salaamu karibu 30 wameshiriki
kikao ambacho pia wamekitumia kueleza changamoto wanazopata wanaposhiriki kutoa
maoni katika vipindi mbalimbali vinavyorushwa na Mpanda Radio.
Baadhi ya wadau wa salaam wakiwa katika chumba cha kurushia matangazo |
Kituo cha Mpanda Radio ambacho ni cha
Kijamii kilianza kurusha matangazo yake mwaka 2013 kikiwa na lengo la kuelimisha,kuhabarisha
na kuburudisha jamii ambapo kilizinduliwa na mwenge wa uhuru Julai 17 mwaka
2013.
source: Issack Gerald
No comments:
Post a Comment